RASIMU YA KATIBA YA MTANDAO WA
MARAFIKI WA ELIMU KANDA YA ZIWA (FENLZ),
TOLEO LA KWANZA 2017.
SEHEMU YA KWANZA:
IBARA YA 1: UTANGULIZI:
Sisi Marafiki wa Elimu wa
Kanda ya ziwa ambao ni muunganiko wa Marafiki wa Elimu waishio katika kanda ya
ziwa kwa hiari yetu tumeamua kujiunga kisheria ili kushughulikia masuala ya
kuboresha Elimu, Demokrasia, Utawala bora na mawasiliano katika jamii ya Kanda
ya ziwa kwa kushirikiana na wananchi wa kada zote na wadau mbalimbali.
Asasi hii imeanzishwa kwa
matakwa ya Marafiki wenyewe kwa lengo la kujihusisha na kuelimisha jamii ili
kuboresha elimu na demokrasia bila shinikizo toka kwa wanasiasa, vikundi vya
dini au ukabila. Asasi hii itatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria za
nchi kanuni na taratibu za mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania.
IBARA YA 2: JINA LA KATIBA NA ANUANI NA UTUMIKAJI:
2.1.Jina la Katiba.
Katiba hii ni waraka halali wa FENLZ, hivyo itajulikana na kutambulika
kwa jina la katiba ya “Marafiki wa Elimu
Kanda ya Ziwa”
2.2. Anuani ya FENLZ itakuwa:-
Mtandao wa Marafiki wa Elimu Kanda ya Ziwa,
S.
L. P Mwanza
2.3.Tarehe rasmi ambayo katiba hii itaanza kutumika.
Katiba hii itaanza kutumika mara baada ya kupata
usajli rasmi na wanachama wa FENLZ na kufanya
uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa katiba hii.
3.
LUGHA YA ASASI:
Kwa kuwa FENLZ
ni asasi huru yenye wanachama wenye viwango tofauti vya elimu; na kwakuwa FENLZ inafanya kazi na watu wa kada
tofauti: lugha kuu ya mawasiliano itakuwa Kiswahili na lugha ya pili itakuwa
Kiingereza
SEHEMU YA PILI:
DIRA,
DHAMIRA, MADHUMUNI NA ULINZI WA ASASI:
4. Dira ya FENLZ:
Nikuwa na Kanda ya ziwa yenye mazingira bora ya
elimu, utawala bora, Demokrasia ya kweli kwa wananchi wote mfumo bora na imara
wa mawasiliano ndani ya jamii.
5.
Dhamira ya FENLZ
Kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi kuhusiana
na changamoto za elimu, Demokrasia na Utawala bora na namna ya kushirikiana na
serikali na jamii kuzikabili changamoto hizo ili kuleta mafanikio chanya kwa
manufaa ya umma.
6. Madhumuni ya FENLZ.
6.1.
Kufanya ufatiliaji na uchambuzi wa masuala ya elimu, demokrasia,
utawala bora na kuimarisha mfumo wa mawasiliano katika jamii na vyombo vya
utawala.
6.2. Kutoa elimu kwa jamii juu
ya umuhimu wa ushiriki wao katika mikutano kwa manufaa ya kijamii na
kukabiliana na changamoto za maendeleo katika maeneo yao.
6.3. Kuendesha midahalo,
mikutano, mijadala, na makongamano ya kijamii juu ya masuala mbalimbali na
kukabiliana na changamoto za maendeleo.
6.4. Kutumia vyombo vya habari
kama redio, TV na magazeti kuelimisha jamii.
6.5. Kujihusisha kikamilifu
katika kusaidia jamii kitaaluma na ushauri katika masuala yanayo kwamisha
maendeleo yao.
6.6. Kutoa elimu kwa jamii
hususani vijana wa shule za Msingi, Sekondari na vyuo pamoja na walio nje ya
shule kuhusiana na haki zao za msingi, elimu ya afya ya uzazi, elimu kuhusiana
na VVU/UKIMWI, magonjwa ya ngono, madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na
sigara, elimu ya ujasiriamali na kuinua kipato, pamoja na masuala mtambuka kama mazingira
6.7. Kutoa elimu ya Demokrasia,
Utawala bora na Usawa wa kijinsia katika jamii.
6.8. Kuanzisha klab za Marafiki
wa Elimu ndani na nje ya shule za Msingi, Sekondari na Vyuo kwa ajili ya
kujadili masuala mbalimbali ya elimu, demokrasia na utawala bora katika jamii.
7.
ULINZI WA ASASI:
Asasi hii itatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa
sheria zilizowekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na
dhamira yake ya kutekeleza shughuli zake
kwa mujibu wa katiba yake na sheria za Tanzania.
SEHEMU YA TATU
KATIBA, USAJILI NA ENEO LA
UTENDAJI KAZI:
8.
Katiba
Katiba ya FENLZ ndio muongozo wa shughuli zote za Asasi hii.
9.
Jina la Asasi
Asasi hii itaitwa MTANDAO WA MARAFIKI WA ELIMU KANDA YA ZIWA kwa kifupisho FENLZ.
10. Usajili
Baada ya kusajiliwa; makao makuu ya FENLZ yatakuwa katika mji wa Mjini
Mwanza katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
11. Eneo la utendaji kazi
FENLZ itafanya kazi katika maeneo ya Kanda
ya Ziwa, kwa kuhusisha ngazi mbalimbali za uanachama na marafiki wa mtandao huu
12. Washirika wa FENLZ.
FENLZ itakuwa na haki ya
kushirikiana na Taasisi, Mashirika mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, watu
binafsi, makampuni na Asasi nyingine ambazo zitakuwa na nia ya kusaidia na kushirikiana na FENLZ katika kutekeleza Dira na Dhamira
ya FENLZ.
13. Kanuni za Kimaadili.
13.1. Katika kutekeleza majukumu
yake; FENLZ itazingatia maadili,
uadilifu, nidhamu, uwajibikaji kujituma, kujitolea na uchapakazi kwa manufaa ya
taifa.
13.2. Wanachama na viongozi wa FENLZ lazima wawe waadilifu.
SEHEMU YA 4:
AINA ZA
UANACHAMA WA FENLZ:
14. UANACHAMA.
Kutakuwa
na aina tatu tu za uanachama wa FENLZ
kwa mujibu wa katiba hii ambazo ni;
14.1Wanachama waanzilishi
Huu ni uanachama wa watu
walishiriki katika kuanzisha wazo la kuundwa kwa FENLZ na ambao kwa namna moja au nyingine walifanikisha FENLZ kupata usajili.
14.2Wanachama
binafsi
14.2.1
Huu ni uanachama wa mtu binafsi ambaye kwa mapenzi yake atapendezwa na
shughuli za FENLZ na kuamua kujiunga
kuwa mwanachama kwa hiari yake mwenyewe.
14.2.2
Kwa mujibu wa katiba hii, kuwa mwanachama wa FENLZ hakuunyimi kuwa mwanachama Wilaya, Mkoa wala Taifa.
14.3Uanachama wa
Heshima
14.3.1
Mtu binafsi, shirika, kampuni au Taasisi yoyote wanaweza kuwa wanachama
wa FENLZ kwa kuchaguliwa /kuteuliwa
na kamati kuu ya uongozi ya FENLZ
kisha kuandikiwa barua ya nia hiyo na iwapo watakubali watakuwa wanachama rasmi
wa FENLZ.
14.3.2
Mwanacham wa heshima wa FENLZ
hatapiga kura ya maamuzi juu ya jambo lolote linalohusu FENLZ.
15. SIFA ZA MWANACHAMA:
15.1
Wanachama waanzilishi
watatambuliwa kwa sifa zifuatazo:
15.1.1
Awe ni mtu aliyejitolea kwa hali na mali katika kuanzishwa kwa FENLZ
15.1.2 Awe na nia ya dhati ya
kuhakikisha kuwa atakuwa mstari wa mbele kutimiza Dira na Dhamira ya FENLZ.
15.1.3
Atambue kuwa anapaswa kuitumikia FENLZ
na si FENLZ imtumikie.
15.1.4
Awe tayari kushirikiana na wadau wengine ili kulinda maslahi ya taifa
15.2
Mwanachama binafsi
15.2.1 Awe ni mtu mwenye kuziunga
mkono kwa dhati shughuli na juhudi za FENLZ
15.2.2 Awe mwenye kujitoa
kuitetea FENLZ ili kufanikisha
malengo yake.
15.2.3 Awe na uwezo wa kuisaidia FENLZ kwa hali na mali pasipo kuchoka.
15.2.4 Awe mtu yeyote mwenye
akili timamu na umri usiopungua miaka kumi na nane (18)
16. HAKI ZA MWANACHAMA
Wanachama wa FENLZ wana haki zifuatazo.
16.1
Kuhudhuria vikao vinavyo wahusu kwa mujibu wa katiba hii.
16.2
Kupata taarifa ya FENLZ kwa
kufuata taratibu zilizopo.
16.3
Kushiriki katika vikao mbalimbali vya maamuzi ya FENLZ kwa mujibu wa taratibu.
16.4
Kuchaguliwa au kuchagua viongozi wa FENLZ kwa mujibu wa wa taratibu za Katiba.
16.5
Haki ya kujitetea na kujieleza kwa tuhuma/kosa alilotenda mbele ya
vyombo vya FENLZ.
16.6
Haki ya kuteuliwa kuiwakilisha FENLZ
katika maeneo/ shughuli mbalimbali.
16.7
Haki ya kupata taarifa na kuzitumia kwa manufaa ya FENLZ na jamii.
16.8
Haki ya kushiriki na kushirikisha uongozi na wanachama wa FENLZ katika mambo yenye manufaa kwa FENLZ na jamii.
16.9
Haki ya kuwa na nakala ya katiba ya FENLZ
17. WAJIBU WA MWANACHAMA:
Wajibu wa mwanachama wa FENLZ ni pamoja na:,
17.1
Kulipa ada na michango yote ya FENLZ
kwa ajili ya uendelevu wa Asasi.
17.2
Kuhudhuria vikao na mikutano yote inayohusu kwa mujibu wa katiba hii.
17.3
Kuwa mwaminifu, mwadilifu mkweli na kutetea msimamo wa FENLZ katika Maendeleo.
17.4
Kuchangia mawazo kwa hali na mali katika kulinda Dira na Dhamira ya FENLZ.
17.5
Kufahamu kwa undani katiba ya FENLZ
18: KUKOMA
UANACHAMA:
Uanachama
utakoma kwa:
18.1
Mtandao wa Marafiki wa Elimu Kanda ya Ziwa kufutwa kwa mujibu wa sheria
za nchi.
18.2
Mwanachama kuamua kujiudhulu kwa hiari yake.
18.3
Kufukuzwa uanachama.
18.4
Kushindwa kulipa ada kwa kipindi cha mwaka mmoja bila sababu za msingi.
18.5
Kukiuka maadili ya uanachama wa FENLZ
kwa makusudi.
18.6
Kwa kutenda kosa lolote ambalo wanachama wataridhia kwamba linafaa
kumuondoa katika uanachama wa FENLZ
na uamuzi huo kuridhiwa na mkutano mkuu.
SEHEMU YA TANO
MUUNDO NA WAJIBU WA VIONGOZI:
19: MUUNDO NA WAJIBU WA VIONGOZI:
Uongozi
wa FENLZ utakuwa kama ifuatavyo
19.1
Mratibu wa FENLZ
19.2
Mwenyekiti wa FENLZ.
19.3
Makamu mwenyekiti wa FENLZ.
19.4
Katibu wa FENLZ.
19.5
Mweka hazina wa FENLZ
19.1 Mwenyekiti
Wajibu wa mwenyekiti utakuwa kama
ifuatavyo:
19.1.1 Mwenyekiti ataongoza
Mikutano ya Bodi ya ushauri na mkutano mkuu wa Wanachama.
19.1.2 Mwenyekiti
atakuwa msemaji mkuu wa FENLZ katika
mikutano ya bodi ya ushauri na mkutano mkuu wa wanachama.
19.1.3 Aache hisia
zake binafsi zikiangalia maamuzi ya wengi ila pale kunapokuwa na usawa wa maamuzi
kwa pande mbili.
19.2
Makamu Mwenyekiti
19.2.1 Makamu mwenyekiti atafanya
kazi za mwenyekiti kama mwenyekiti hayupo.
19.2.2
Atafanya kazi za mwenyekiti kwa kuagizwa na mwenyekiti
19.2.3
Kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya mikutano ya bodi ya ushauri na
mkutano mkuu wa FENLZ.
19.3
Katibu
Katibu
atakuwa na kazi zifuatazo;
19.3.1
Atatunza kumbukumbu za vikao vya bodi ya ushauri na mikutano ya FENLZ.
19.3.2
Ndiye katibu wa mikutano ya kamati ya Bodi ya Ushauri na mkutano mkuu
wa FENLZ.
19.3.3
Katibu atawasiliana na mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa maamuzi ya utekelezaji.
19.3.4
Kuandika barua na kuitisha vikao baada ya kuwasiliana na mwenyekiti.
19.3.5
Kuandaa agenda za mikutano ya Bodi ya Ushauri, Mkutano mkuu na mikutano
ya Dharula.
19.3.6
Kuandaa taarifa mbalimbali za FENLZ
na kuzipeleka pale zinapo hitajika
19.3.7
Kuratibu shughuli mbalimbali za kamati ndogo ndogo za FENLZ.
19.3.8
Kuratibu shughuli zote za kila siku za FENLZ.
19.4
Mweka Hazina
19.4.1
Mweka hazina atakuwa na wajibu ufuatao;
19.4.2
Atakuwa mtunzaji mkuu wa fedha za FENLZ.
19.4.3
Atasimamia utunzaji wa vitabu vya kumbukumbu za fedha za FENLZ.
19.4.4 Kuaandaa na kutoa taarifa
za fedha za FENLZ katika vikao vya
Bodi ya Ushauri na Mkutano mkuu wa FENLZ.
19.4.5
Atakuwa mdhamini wa mali za Asasi kwa niaba ya FENLZ
19.4.6
Kushughulikia suala la utafutaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya
uendelevu wa FENLZ.
19.5
Mratibu wa FENLZ
19.5.1 Ndiye mratibu mkuu wa shughuli zote za FENLZ
19.5.2 Ndiye mkuu wa idara ya
utafiti na mawasiliano ndani ya FENLZ
SEHEMU YA 6
UCHAGUZI NA
MUDA WA KUKAA MADARAKAN.
20.
Muda wa Uongozi
Viongozi watakao chaguliwa
kwa mujibu wa katiba hii watadumu madarakani kwa muda wa miaka miwili (2),
lakini wanaweza kuchaguliwa tena kwa kiindi kingine.
21.
SIFA ZA KIONGOZI:
21.1.
Awe mwanachama wa FENLZ
21.2.
Awe na uwezo wa uongozi na kupambanua mambo
21.3.
Awe mwenye sifa na uwezo wa uongozi
21.4.
Mwenye kujituma
21.5.
Anaye kubali kutoa na kupokea ushauri toka kwa watu wengine walio
wanachama na wasio wanachama wa FENLZ
na kuufanyia kazi.
21.6.
Awe tayari kujitolea kuliko kutegemea mapato/ malipo toka FENLZ.
22. KUONDOKA KATIKA UONGOZI:
Viongozi
wanaweza kuondoka madarakani kwa njia zifuatazo;
22.1.
Kutokuchaguliwa tena na wanachama
22.2.
Kujiuzulu
22.3.
Kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na wanachama
22.4.
Kufukuzwa kutokana na makosa ya kukiuka katiba hii
22.5.
Kuhukumiwa kifungo jela kwa makosa ya jinai n.k
22.6.
Kupata maradhi ambayo yataathiri kabisa uwezo wake wa kutekeleza
majukumu yake ya kila siku.
22.7.
Kufariki dunia.
22.8.
Kuhama makazi ya kudumu nje ya maeneo ya kanda ya ziwa
SEHEMU YA SABA
MIKUTANO NA
VIKAO VYA FENLZ:
23. MIKUTANO/VIKAO VYA FENLZ NA MAJUKUMU YAKE.
FENLZ Itakuwa na Mikutano/vikao kama
ifuatavyo;
23.1.
Mkutano Mkuu
23.1.1.
Kutakuwa na mkutano mkuu wa wanachama ambao utafanyika mara moja kila mwisho wa mwaka.
23.1.2.
Mkutano utahudhuliwa na watendaji wote wa FENLZ, wanachama hai (waliolipa
Kiingilio na ada), wanachama waanzilishi wa FENLZ, wanachama wa heshima na
wageni mbalimbali watakao alikwa kuhudhuria.
23.1.3.
Mkutano mkuu ndio chombo chenye madaraka yote ya kuamua mambo muhimu ya
FENLZ ikiwa ni pamoja na kupitisha
sera na taratibu mbalimbali za kusimamia uendeshaji wote wa Asasi.
23.1.4.
Kuchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti, mweka hazina, na wajumbe wa
bodi ya ushauri ya FENLZ pamoja na
wajumbe wa kamati mbalimbali.
23.1.5.
Kupokea na kupitisha makisio ya mapato na matumizi ya FENLZ kutoka kwa mweka hazina.
23.1.6.
Kupitisha jina la mkaguzi wa mahesabu ya FENLZ.
23.1.7.
Kujadili na kupitisha taarifa za mwaka za utekelezaji wa shughuli za FENLZ.
23.1.8.
Kujadili na kupitisha mabadiliko ya katiba ya FENLZ.
23.1.9.
Kujadili na kupitisha mikakati na mipango ya muda mfupi na mrefu ya FENLZ.
23.1.10. Kufanya maamuzi yote ya FENLZ, kama itakavyo onekana inafaa.
23.2.
Mkutano Mkuu wa dharura
23.2.1. Mkutano wa dharura unaweza
kuitishwa endapo kutakuwa na ombi lililotolewa na kutiwa saini na si chini ya
theluthi mbili (2/3) idadi ya wanachama na kuweka bayana katika ombi hilo suala
ambalo limesababisha kuitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura.
23.2.2. Mkutano Mkuu wa dharura
utahudhuliwa na watendaji wote wa FENLZ,
wanachama hai (waliolipa ada na kiingilio), wanachama waanzilishi, wanachama wa
heshima na wageni waalikwa.
23.2.3. Mkutano Mkuu wa dharura
unaweza kuitishwa mara moja tu (1) kwa mwaka.
24. UENDESHAJI WA VIKAO:
24.1. Taarifa ya mkutano mkuu wa
kawaida itatolewa kwa kila mwanachama si chini ya siku kumi na nne (14), na taarifa ya mkutano mkuu wa
dharura itatolewa kwa wanachama si zaidi ya siku saba (7), kabla ya siku ya mkutano husika.
24.2. Wanachama watakaotaka
kuleta mawazo/ agenda maalumu kwenye Mkutano Mkuu, watatoa taarifa ya maandishi
kwa katibu wa FENLZ siku saba kabla
ya siku ya mkutano.
24.3. Nusu ya idadi ya wanachama
halali wa mkutano mkuu watakamilisha akidi (Quorum) ya mkutano wowote ule
isipokuwa kwamba akidi haitahitajika endapo Mkutano umetokana na mkutano
ulioahirishwa; endapo wanachama watakao kuwepo watachukuliwa kutosheleza akidi.
24.4. Katika mkutano unaotokana
na mkutano ulioahirishwa hautaruhusiwa kufanya maamuzi yoyote ya kubadili
katiba ya FENLZ.
24.5. Endapo saa moja na nusu
itapita tangu muda uliokubaliwa kuwa ndio wa kuanza mkutano bila idadi ya
wajumbe kutimia ili kuweza kufanya mkutano; basi mkutano uta ahirishwa na Mwenyekiti
au makamu mwenyekiti hadi siku kama hiyo wiki inayofuata.
24.6. Mwenyekiti ndiye
atakayeongoza mikutano ya Kamati ya Utendaji, Mkutano Mkuu na Mkutano Mkuu wa
dharura.
24.7. Makamu mwenyekiti
ataongoza shughuli za mikutano kama mwenyekiti hayupo.
24.8. Endapo Mwenyekiti na
makamu mwenyekiti hawakuhudhuria basi mjumbe mmoja anaweza kupendekezwa kuwa
mwenyekiti kwa wakati huo.
24.9. Katika mkutano mkuu
maamuzi yatatokana na kupiga kura kwa kuinua mikono juu isipokuwa kama
wanachama walioko katika mkutano wanaamua kwamba kura zipigwe kwa siri (secret
ballot).
24.10. Uamuzi utaonekena kuwa
umepitishwa kwa idadi ya wingi wa kura kuunga mkono hata kama tofauti ni ya
kura moja (Majority decision) isipokuwa kama kura ni kwa ajili ya kubadili katiba basi kura ni lazima ziwe siyo
chini ya theluthi mbili (2/3) ya idadi ya wanachama waliohudhulia kukubali.
24.11. Hakutakuwepo na upigaji
kura ya uwakilishi (no voting by proxy)
24.12. Katika upigaji kura endapo
kura zitafungana Mwenyekiti atakuwa na kura ya Mwisho (Casting vote
24.13. Ni budi Mwenyekiti
aheshimiwe wakati wa mkutano
24.14. Uamuzi wa mwenyekiti
katika kudhibiti mwenendo wa mkutano ni wa mwisho labda kama atapingwa na
theluthi ya wajumbe.
24.15. Mwenyekiti anamamlaka ya
kuingilia usumbufu wowote unaojitokeza wakati wa Mkutano au kumtoa nje mjumbe
ambaye anasumbua mwenendo wa mkutano.
24.16. Mjumbe atakayetolewa nje
kwa ajili ya usumbufu atatakiwa aondoke eneo la Mkutano.
SEHEMU YA NANE.
- SHERIA
NDOGO ZA ASASI
25.1.
Mwanakikundi anatakiwa kuudhuria shughuli zote za kikundi.
25.2.
Simu ikiita kwenye kikao mwanachama atatozwa shilingi 500/=.
25.3.
Kudanganya faini ni shilingi 5000/=
25.4.
Kuchelewa kufika kwenye kikao faini ni shilingi 500/=
25.5.
Kupiga kelele au kuongea bila ruhusa ya kiongozi shilingi 1000/=
25.6.
Kutoudhuria kikao kimoja faini ni shilingi 500/=
25.7.
Mwanachama atakaye shindwa kulipa ada na michango katika kipindi cha
mwaka mmoja atakuwa amejifukuza mwenyewe
25.8.
Kuwa mwaminifu, mwadilifu mkweli na kutetea msimamo wa FENLZ katika Maendeleo.
25.9.
Kuchangia mawazo kwa hali na mali katika kulinda Dira na Dhamira ya FENLZ.
25.10.
Kukiuka maadili ya uanachama wa FENLZ
kwa makusudi kutasababisha kusimamishwa au kuvuliwa uanachama wa FENLZ
25.11.
Kwa kutenda kosa lolote ambalo wanachama wataridhia kwamba linafaa
kumuondoa katika uanachama wa FENLZ
na uamuzi huo kuridhiwa na mkutano mkuu.
25.12.
Mwanachama atakaye fariki ndugu zake watapewa asilimia thelathini (30%)
ya michango yake ya mwaka mmoja.
25.13.
Mwanachama atakaye hama eneo atapewa asilimia thelasini (30%) ya
michango yake ya mwaka mmoja
SEHEMU YA TISA
MAPATO NA USIMAMIZI WAKE
26.
MAPATO, UHIFADHI NA UTOAJI
WA FEDHA BENKI:
26.1. Mapato ya FENLZ yanatokana na ada za uanachama,
ada za kiingilio, michango ya wanachama, ruzuku na misaada ya wafadhili/
wahisani mbalimbali wa FENLZ.
26.2. Mwaka wa fedha wa FENLZ utaanza tarehe 1 Januari na
kuishia tarehe 31 Desemba ya kila mwaka
26.3. Fedha zote za FENLZ zitawekwa katika tawi la benki
litakalokuwa limeteuliwa isipokuwa fedha za matumizi madogomadogo zisizozidi 50,000/= zitahifadhiwa kwenye ofisi ya FENLZ (Kama Petty Cash).
26.4. Waweka saini benki
watakuwa wanne (4) ambao ni Mwenyekiti, Muhasibu na wajumbe wawili watakao
chaguliwa na Bodi yaUshauri ambapo kati yao wawili watakuwa kundi “A”na wawili watakuwa
kundi “B”.
26.5. Fedha zitatolewa benki kwa
kusainiwa na watu wawili mmoja kutoka kundi A na mmoja kutoka kundi B.
SEHEMU
YA KUMI:
MABADILIKO
YA KATIBA, KUVUNJIKA NA LAKIRI YA ASASI.
27. MABADILIKO YA KATIBA, KUVUNJA NA LAKIRI YA ASASI:
27.1.Mabadiliko ya Katiba:
Katiba haiwezi kubadilishwa au kufanyiwa
marekebisho kwa namna yoyote ile isipokuwa kwa uamuzi utakao kuwa umefikiwa
katika Mkutano Mkuu maalumu wa wanachama ambao utahudhuriwa na si chini ya
theluthi mbili ya wanachama.
27.2.Kuvunjika kwa Asasi
27.2.1. FENLZ itafikia ukomo kwa kuvunjika kama uamuzi huo utafikiwa na theluthi
mbili ya wanachama waliohudhuria Mkutano Mkuu kupiga kura za kukubali uamuzi
huo.
27.2.2. Kama Mkutano utaazimia
kuvunjika kwa FENLZ; utafanya
utaratibu wa kulipa madeni yote ya FENLZ
na hatimaye kumilikisha mali za FENLZ
kwa asasi yenye makao yake mjini Katoro na yenye malengo yanayofanana na ya
Asasi hii.
28. MUHURI NA NEMBO YA FENLZ:
28.1.Kutakuwa na muhuri wa
Asasi ambao ni wa duara na ndani yake utasomeka MARAFIKI WA ELIMU KANDA YA ZIWA
na katikati ya maneno hayo kutakuwa na anuani ya FENLZ, S.L.P. MWANZA.
28.2.Nembo ya FENLZ.
28.2.1. Nembo ya utambulisho ya FENLZ itakuwa na watu wazima wawili wa
jinsia zote walioshikana mikono kuwafunika watoto wawili wa jinsia zote na
nyuma ya watoto kutakuwa na kitabu chenye kalamu katikati.
28.2.2. Maana ya kuwa na alama
hizi ni kwamba kwa kuwa na elimu; kutakufanya kuona mbali, kuwa na upeo mzuri
wa matumizi ya anga, kutumia vyema rasilimali za nchi kavu na majini kwa
manufaa ya Taifa.
28.2.3. Kwenye nembo hiyo kutakuwa
na maneno yanayosomeka Mtandao Wa
Marafiki Wa Elimu Kanda ya Ziwa *Friends
Of Education Network Lake Zone (FENLZ).
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
MENGINEYO:
29. UWEZO WA KUJIUNGA NA TAASISI NYINGINE:
FENLZ inaweza kujiunga na Asasi
ama Taasisi nyingine kwa kadri inavyofaa ili mradi uamuzi wa kujiunga na
Taasisi au mitandao utaafikiwa na Bodi na wanachama watapata taarifa hizo
kupitia kwenye Mkutano Mkuu.
30. UTATUZI WA MIGOGORO:
Mgogoro wowote ndani ya FENLZ
utakaoshindikana kupata usuluhishi ndani ya FENLZ, utaamuliwa na wanachama wa FENLZ katika Mkutano Mkuu na huo ndio utakuwa na madaraka na
maamuzi ya mwisho.
UTHIBITISHO:
Sisi ambao majina yetu yameorodheshwa hapa chini
na kutiwa saini zetu ndio wanachama waanzilishi wa Asasi ya Marafiki wa Elimu
Kanda ya Ziwa (FENLZ) mwaka 2017. Kwa
kutambua kuwa jamii inategemea juhudi za watu mbalimbali wenye ushirikiano ili
kuleta maendeleo; tumeamua kwa ridhaa yetu kufanya uamuzi wa kuanzisha Asasi
hii ambayo itafanya kazi kwa ushirikiano na jamii, wataalam mbalimbali na wadau
kutoka serikalini na wadau wa nje ili kufikia malengo ya FENLZ na maendeleo ya Taifa.
Tutailinda, kuiheshimu, kuitetea na kuitunza
Katiba hii ili itekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu
za kisheria za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
No
|
JINA
|
SAINI
|
1
|
|
|
2
|
|
|
3
|
|
|
4
|
|
|
5
|
|
|
6
|
|
|
7
|
|
|
8
|
|
|
9
|
|
|
10
|
|
|
TUNATHIBITISHA KWAMBA HII NI NAKALA HALISI YA KATIBA YA FENLZ
**********************************************************************