Kurasa

Jumamosi, 11 Novemba 2017

MARAFIKI WA ELIMU GEITA WAKABIDHI VYETI

MARAFIKI WA ELIMU GEITA WAKABIDHI VYETI
VYA USHIRIKI KWA WANACHUO

Asasi ya Marafiki wa Elimu Geita imewatunuku vyeti vya uanachama wawajibikaji wanachuo watano kutoka Chuo cha Ufundi Stadi cha Geita VTC. Wanachuo hao ni wahitimu wa mwaka wa pili ambao ni wale waliokuwa wamejiunga na klabu ya Marafiki wa Elimu katika chuo hicho cha Ufundi Stadi cha Geita VTC.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 35 chuoni hapo Padre Hendrick Tibiyabo mara baada ya kukabidhi vyeti hivyo na vinginevyo aliwaasa wanachuo kuendelea na moyo wa kujituma hata kule wanako kwenda kwani ndio siri ya mafanikia na pia kwa wale wanaobakia wakazanie sana masomo yao na kuzingatia kile wanacho fundishwa na kuelekezwa na walimu wao.

Miongoni mwa wanachuo waliokabidhiwa vyeti hivyo uwajibikaji ndani ya Klabu hiyo ya Marafiki wa Elimu ni
1.  Jumanne Yussuf Mussa – ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo ya Marafiki wa Elimu chuoni hapo
2.  Rayton Wasiwasi – ambaye ni Katibu wa Klabu hiyo ya Marafiki wa Elimu
3.  Tasiana Kime – aliye kuwa ni Mwekahazina wa Klabu ya marafiki wa Elimu
Wengine waliopokea vyeti hivvyo ni Baraka Hamadi Hamidu na Thobias Venac ambao wote ni wahitimu wa masomo yao ya ufundi chuoni hapo kupitia fani mbalimbali kama vile za umeme wa majumbani, viwandani na umeme wa Magari pia fani ya Uhazili (Secretarial) na fani nyinginezo zinazo tolewa na chuo hicho.

Maoni ya wanachuo hao mara baada ya kupokea vyeti hivyo waliendelea kuwaasa wale wengine wanaobakia kuiendeleza vema Klabu na kuzingatia masomo yao. Pia Mwenyekiti wa Klabu hiyo ya Marafiki wa elimu (Jumanne Yussuf Mussa) alitoa shukrani kwa asasi hiyo ya marafiki wa Elimu Geita iliyokuwa chini ya Mkurugenzi wake ndugu Ayubu Bwanamadi yenye makao makuu yake Geita Mjini



Wanaklabu ya Marafiki wa Elimu Chuo cha Ufundi Geita wakiwa na vyeti vyao vya ushiriki na uwajibikaji walivyo tunukiwa na asasi ya Marafiki wa Elimu Geita (FENG) . Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo ndugu Ayubu Bwanamadi akifuatiwa na Rayton Wasiwasi ambaye ni Katibu wa Klabu akifuatiwa na Jumanne Yussuf Mussa ambaye ni Mwenyekiti  akifuatiwa na Thobias Venac. Aliye chuchumaaa ni Tasiana Kime aliyekuwa ni Mwekahazina wa Klabu hiyo na wakwanza kulia ni Baraka Hamadi Hamadi




MARAFIKI WA ELIMU GEITA
S. L. P 45 GEITA
+255 742 354 689
marafikiwaelimugeita@gmail.com
nyuma ya msikiti wa Ijumaa mjini Geita
inatazamana na Storm FM redio

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni