Kurasa

Jumamosi, 11 Novemba 2017

MARAFIKI WA ELIMU GEITA WATOA MSAADA KWA WATOTO

MARAFIKI WA ELIMU GEITA WATOA MSAADA KWA WATOTO 
WANAOLELEWA NA KITUO CHA BRIGHTLIGHT ORGANIZATION

kufuatia ghafla iliyo fanyika katika hoteli ya Omega ambapo Marafiki wa Elimu ni moja ya waalikwa na wadau wa karibu wa asasi hiyo waliguswa na changamoto zinazo wakabili watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho.

pamoja na kutoa michango ya kifedha pia asasi ya MARAFIKI WA ELIMU GEITA ilifanikiwa kukabidhi mfuko mmoja wa sabuni ya unga kwa watoto hao chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa asisi hiyo ya Brightlight ndugu Mathew Daniel. Asasi ya Marafiki wa Elimu Geita iliwakilishwa na bi Amina Mvungi ambaye ndiye Mwekahazina wa FENG aliye ambatana na Samson Philipo Katibu msaidizi Athmani Kyatanga mjumbe wa bodi ya ushauri pamoja na Mkurugenzi wa asisi hiyo ndugu Ayubu Bwanamadi

katika salamu na shukrani kwa watoto hao waliomba pia washirika na wadau wengine kuwatembelea ili kuweza kujua mahitaji yao ambapo ni pamoja na upatikanaji wa matibabu ya uhakikaka ili kutunza afya zao.

pia uongozi wa kituo hicho cha Brightlight kilitoa shukrani nyingi kwa uongozi na wajumbe wote wa asasi ya Marafiki wa Elimu Geita (FENG) kwa kuguswa kwa hali moja hadi nyingine na kukubali kushiriki pamoja na watoto hao katika chakula pamoja na msaada wao waliotoa


MARAFIKI WA ELIMU GEITA
+255742 354 689
marafikiwaelimugeita@gmail.com
nyuma ya msikiti wa Ijumaa
tunatazamana na Storm FM redio



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni