MARAFIKI
WA ELIMU GEITA WAKABIDHI VYETI
VYA
USHIRIKI KWA WANACHUO
Asasi ya Marafiki wa Elimu Geita imewatunuku vyeti vya uanachama
wawajibikaji wanachuo watano kutoka Chuo
cha Ufundi Stadi cha Geita VTC. Wanachuo hao ni wahitimu wa mwaka wa pili
ambao ni wale waliokuwa wamejiunga na klabu ya Marafiki wa Elimu katika chuo
hicho cha Ufundi Stadi cha Geita VTC.
Mgeni Rasmi katika Mahafali
ya 35 chuoni hapo Padre Hendrick Tibiyabo mara baada ya
kukabidhi vyeti hivyo na vinginevyo aliwaasa wanachuo kuendelea na moyo wa
kujituma hata kule wanako kwenda kwani ndio siri ya mafanikia na pia kwa wale
wanaobakia wakazanie sana masomo yao na kuzingatia kile wanacho fundishwa na
kuelekezwa na walimu wao.
Miongoni mwa wanachuo
waliokabidhiwa vyeti hivyo uwajibikaji ndani ya Klabu hiyo ya Marafiki wa Elimu
ni
1. Jumanne Yussuf Mussa –
ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo
ya Marafiki wa Elimu chuoni hapo
2. Rayton Wasiwasi –
ambaye ni Katibu wa Klabu hiyo ya
Marafiki wa Elimu
3. Tasiana Kime –
aliye kuwa ni Mwekahazina wa Klabu
ya marafiki wa Elimu
Wengine
waliopokea vyeti hivvyo ni Baraka Hamadi
Hamidu na Thobias Venac ambao
wote ni wahitimu wa masomo yao ya ufundi chuoni hapo kupitia fani mbalimbali
kama vile za umeme wa majumbani, viwandani na umeme wa Magari pia fani ya
Uhazili (Secretarial) na fani nyinginezo zinazo tolewa na chuo hicho.
Maoni ya wanachuo hao mara
baada ya kupokea vyeti hivyo waliendelea kuwaasa wale wengine wanaobakia
kuiendeleza vema Klabu na kuzingatia masomo yao. Pia Mwenyekiti wa Klabu hiyo
ya Marafiki wa elimu (Jumanne Yussuf Mussa) alitoa shukrani kwa asasi hiyo ya
marafiki wa Elimu Geita iliyokuwa chini ya Mkurugenzi wake ndugu Ayubu
Bwanamadi yenye makao makuu yake Geita Mjini
Wanaklabu ya
Marafiki wa Elimu Chuo cha Ufundi Geita wakiwa na vyeti vyao vya ushiriki na
uwajibikaji walivyo tunukiwa na asasi ya Marafiki wa Elimu Geita (FENG) . Wa pili kutoka kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo ndugu Ayubu
Bwanamadi akifuatiwa na Rayton
Wasiwasi ambaye ni Katibu wa
Klabu akifuatiwa na Jumanne Yussuf Mussa
ambaye ni Mwenyekiti akifuatiwa na Thobias Venac. Aliye chuchumaaa ni Tasiana Kime aliyekuwa ni Mwekahazina
wa Klabu hiyo na wakwanza kulia ni Baraka
Hamadi Hamadi
MARAFIKI WA ELIMU GEITA
S. L. P 45 GEITA
+255 742 354 689
marafikiwaelimugeita@gmail.com
nyuma ya msikiti wa Ijumaa mjini Geita
inatazamana na Storm FM redio