MFAHAMU MRATIBU WA MTANDAO WA MARAFIKI WA ELIMU GEITA (MMEG/FENG) FRIEND’S OF EDUCATION
NETWORK GEITA
AYUBU MZEE
BWANAMADI ni kijana mwenye umri wa
miaka 29. Amezaliwa katika wilaya ya Pangani
mkoani Tanga nchini Tanzania Julia 1987.
ELIMU
Ameanza kusoma shule ya msingi Funguni wilayani
Pangani mwaka 1996 na kuhitimu elimu
yake ya msingi mwaka 2002. Na baada
ya hapo kufanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari
FUNGUNI na kuhitimu kidato cha nne mnamo mwaka 2006. Baada ya hapo alijiunga na
chuo cha mkoa cha ufundi stadi na huduma cha (RVTSC) VETA TANGA kwa upande wa
fani ya uhazili na Tarakilishi (secretarial and Computer Course) kwa kipindi
cha 2009 hadi 2010 kwa kuhitimu hatua ya tatu..
Baada ya hapo alijunga na chuo cha ualimu wa ufundi
kilichopo mkoa Morogoro Morogoro
Vocational Teachers Training Collage (MVTTC) kwa kipindi cha masomo 2012/2013.
KAZI.
BWANAMADI alifanikiwa kufanya kazi kwa kujitolea
katika halmashauri ya wilaya ya Pangani kama Katibu Muhtasi katika ofisi ya
utumishi wilayani hapo kwa kipindi cha Desemba 2010 hadi april 2011. Pia
alifanya kazi katika kampuni ya uuzaji na usambazaji bidhaa ya Apex Market iliyokuwa jijini Tanga mtaa wa
Majani Mapana mwaka 2007. Pia sehemu nyingine ya kazi ambapo amefanya kazi ni
katika chuo cha ufundi stadi na huduma VETA Geita kuanzia mwaka 2014 Januari
hadi 2016.
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU
Bwanamadi alijiunga na harakati za Marafiki wa Elimu mnamo
mwaka 2005 akiwa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Funguni iliyopo
wilayani Pangani mkoani Tanga. Kwa zaidi ya miaka kumi kuanzia mwaka 2005 amekuwa akiendeleza
Harakati za marafiki wa elimu. Kilichomvutia kujiunga na harakati hizi ni
matangazo yaliyo kuwa yakirushwa na vyombo vya habari (video) ambayo mwisho
yalikuwa yakileta hamasa kwa jamii kutaka kujua kipi kinacho endelea. Pamoja na
vidokezo vya uelimishaji vilivyokuwa vikielimisha jamii kulikuwa na ujumbe
usema “tuandikie rafiki@hakielimu.org”. Pamoja na anuani
ya sanduku la barua kwa njia ya posta.
LENGO LA KUJIUNGA NA HARAKATI
Miongoni mwa malengo
yaliyompelekea Bwanamadi kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu yalikuwa ni
1.
kuungana
na wadau wengine wa elimu katika kuleta maendeleo chanya katika Nyanja hii ya
elimu
2.
Kutoa
elimu kwa jamii kadri ya muda na fursa inavyo patikana.
3. Kusaidia jamii yenye
uhitaji kadri ya muda na uweze atakao kuwanao.
MAFANIKIO
Katika uwepo wake
ndani ya harakati hizi za marafiki wa elimu Bwanamadi amepata mafanikio mengi
ikiwa ni kupata namba ya uanachama (membership number membership No: 318727)
kutoka shirika la HakiElimu lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam ambalo
ni ndio Mraghabishi mkuu wa harakati za Marafiki wa Elimu Tanzania. Miongoni
mwa mafanikio mengine ni:
a) Kuhamasisha wengine kujiunga na harakati hizi za marafiki wa
elimu jambo ambalo ninaendelea kulifanya hadi sasa
b)
Kutoa
elimu kupitia vyombo vya habari (redio na magazeti kama vile gazeti la Rai
ambapo moja ya mada ilisema “kidole
kimoja….” Mada ambayo ilikuwa ikihamasisha jamii kushiriki kikamilifu
katika ujenzi wa shule za kata na
gazeti la Mwananchi kwa mada isemayo “ Ikibidi mitaala ibadilishe baada ya miaka
kumi” na redio ya Breeze FM na Mwambao FM zilizopo mkoani Tanga, Abood FM
iliyopo mkoani Morogoro na Redio ya Storm FM iliyopo mkoani Geita.
c)
Kuanzisha
maktaba ya jamii ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Mmadi Maktaba ambapo baadaye ilikuwa ikisimamiwa na kikundi cha
marafiki wa elimu (Mwangaza Gombero)
kilichopo kitongoji cha Gombero kata ya Pangani Mashariki wilayani Pangani
mkoani Tanga.
d)
Kuwa
ni mmoja wa waanzishi wa mitandao ya marafiki wa elimu nchini kwa kuanzisha mtandao
wa kwanza wa marafiki wa elimu mkoani Tanga ambao ulikuwa ni mtandao wa
marafiki wa elimu wilayani Pangani
e)
Kutembelea
shuleni kufanya tafiti ya kubaini hali ya wanaochaguliwa kujiunga kidato cha
kwanza bila kujua kusoma kuandika na kuhesabu (kkk) na hii aliambatana na marafiki wa elimu kutoka kikundi cha
marafiki wa elimu cha Mwangaza gombero huko wilayani Pangani. Pia kupima mpango
wa matokeo makubwa sasa BRN na hii
alikuwa mkoani Geita ambapo aliambatana na Marafiki wa Elimu Geita pamoja na
wafanyakazi kutoka shirika la HakiElimu ambao ni Mr. Alinanuswe Kasyele, Mr.
Raphaeli Kalonga na Mr. Pius
Makomelelo ambapo ilikuwa ni mwaka 2015
na kushiriki na kuratibu zoezi la tafiti ya uwajibikaji na ushiriki wa wananchi
katika maendeleo ya elimu katika maeneo ya Halmashauri ya Mji Geita mkoani
Geita mwaka 2016.
f)
Kuwa
kiongozi katika mitandao tofauti ya marafaki wa elimu kwa nafasi ya katibu wa mtandao wa marafiki wa elimu
wilayani Pangani chini ya mwenyekiti Mzee
Magendo (Kisport), Makamo Mwenyekiti
wa mtandao wa mkoa wa marafiki wa elimu wa mkoa Tanga chini ya mwenyekiti mama Mariamu Makoko. Mshauri wa mtandao wa marafiki wa elimu wilayani na mkoani Morogoro
chini ya mwenyekiti Islamu Khasim Mposo. Katibu wa marafiki wa elimu Geita mji chini ya mwenyekiti ndugu Patrick Boniphace Mabula na hatimaye
kuwa Mratibu wa mtandao wa marafiki
wa elimu wilayani Geita chini ya mwenyekiti ndugu Alex Rwigi Kadaraja.
g)
Kuanzisha
kilabu ya wapinga rushwa katika chuo cha ufundi stadi na huduma cha VETA TANGA.
h)
Kuwa
Rais katika serikali ya wanachuo
katika chuo hicho cha VETA TANGA.
i)
Kuwasaidia
watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo zoezi hili
alifanya akiwa na kikundi cha Mwangaza
Gombero chini ya mwenyekiti wake bi Amina Abdallah
j)
Kuhamasisha
wanajamii walioanzisha vikundi ili kujiunga na harakati hizi na kupata marafiki
wapya katika kijiji cha Katoro na Kamena wilayani Geita.
k)
Kupata
nafasi ya kusimamia zoezi la utafiti juu ya uelewa kwa watoto lililokuwa
likiendeshwa na asasi ya Uwezo na
kuwa msimamizi msaidizi wilayani Pangani
mwaka 2012
l)
Pia
alitumia nafasi yake ya kazi na kufanikiwa kuanzasha klabu ya marafiki wa elimu
katika chuo cha ufundi stadi cha Geita (Geita Vocational Training Centre) klabu
ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa mtandao wa marafiki wa elimu Geita ambapo
kupitia klabu Mtandao wa Marafiki wa Elimu Geita (MMEG) uliweza kuandaa maeneo
ya kufanyia vikao tofauti vya mtandao wa marafiki wa elimu Geita. Kuibua
changamoto zinazo wakabili wanafunzi na kuzijadili kwa pamoja.
m)
Kushiriki
katika kuandaa katiba ya mtandao wa marafiki wa elimu na kufanikisha usajili wa
mtandao wa marafiki wa elimu Geita Friend’s of Education Network Geita
(MMEG/FENG) kwa hatua ya asasi za kijamii (Community Based Organization –CBO) ngazi ya wilaya kwa kupatiwa cheti
cha usajili na kusajiliwa kwa namba CBO.01335
katika halmashauri ya mji Geita.
CHANGAMOTO
“ni
kweli kwamba kila jambo linachangamoto zake lakini kwangu changamoto katika
harakati za marafiki wa elimu sizioni kuwa ni vikwazo vya kunizuia kufanya
jambo nililolipanga bali huwa ni fursa ya ya kuniwezesha kutafaka njia mbadala
ya kuweza kufika pale ninapo hitaji au kufanikisha lile ambalo nimelipanga.
MIKAKATI.
1.
Kujiimarisha
vema katika harakati za marafiki wa elimu popote pale nitakapo kuwa katika
utafutaji au matembezi ya kawaida kwa kujenga mahusiano ya karibu na wadau wa
elimu na wanajamii kwa ujumla.
2.
Kuendeleza
mtandao wa marafiki wa elimu Geita pamoja na mitandao mingine itakayo hitaji
msaada wake kwa hali na mali ili kuisadia jamii katika maendeleo ya elimu.
3.
Kuendeleza
harakati ndani ya mtandao wa marafiki wa elimu Geita na mitandao mingine hadi
kufikia hatua ya asasi isiyo ya kiserikali (Non Government Organization – NGO)
4.
Kujenga
ushawishi kwa jamii na viongozi kujiunga na harakati za marafiki wa elimu na
kuwa na mtazamo chanya katika maendeleo ya elimu katika maeneo yao.
OMBI
Ninawaomba marafiki
wa elimu bila kujalisha mtaa, kitongoji,
kata, wilaya, mkoa ama tunatokea kanda gani tushirikiane vema katika kuleta
maendeleo chanya juu ya elimu na demokrasia.
Pia ninaiomba jamii
hususan walezi na wazazi kufuatilia vema maendeleo ya watoto wao (wanafunzi)
wawapo maeneo ya shule ama nje ya shule zao kimaadili na kimazingira ili kuweza
kuwasaidia wanafunzi na walimu kuinua taaluma za watoto (wanafunzi) hao.
Pia jamii ninaiomba
kusoma machapisho yanayohusiana na masuala ya elimu ili kuweza kufahamu vema
mahitaji na maendeleo ya elimu katika jamii zao
Pia ninaiomba
serikali kuandaa falsafa ya elimu ya nchi yetu ya Tanzania kwa kipindi hiki
tulichonacho ili kila mmoja aliyekuwa masomoni au nje ya masomo ajue kuwa
anasoma kwa kutumia falsafa gani ya nje yake kama vile ilivyokuwa kwa wakati wa
awamu ya kwanza “ujamaa na kujitegemea”
Mungu ibariki
HakiElimu na wafanyakazi wake. Zibariki harakati za elimu na marafiki wake.
Ibariki nchi yetu pendwa ya Tanzania.
MAWASILIANO
Ayubu M. Bwanamadi
Mratibu wa Mtandao wa Marafiki
wa Elimu Geita
S. L. P 45 Geita
Simu: +255765384115/+255714771883
B-Pepe: bwanamadiam@yahoo.com
XXXXXXXXXX DESEMBA 2016 XXXXXXXXXX
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni