MARAFIKI WA ELIMU GEITA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU SAM
Marafiki wa elimu kutoka Mtandao wa Marafiki wa Elimu Geita wamepatiwa mafunzi juu ya ufuatiliaji na utekelezaji mpango wa kuelimisha na kuhamasisha jamii kushiri na kuwajibika vema katika maendeleo ya elimu wilayani geita.
Marafiki wa Elimu Geita wamepatiwa uwezo kwa muda wa siku tatu na kutekeleza zoezi hilo kwa muda wa siku kumi na mbili (12) ambapo mafunzo hayo yaliendeshwa chini ya usimamizi wa shirika la HakiElimu ambapo walishirikiana vema na The Foundation for Civil Society
marafiki wa elimu walipata fursa ya kutembelea baadhi ya shule za msingi na sekondari zilizopo ndani ya Halmashauri ya Mji Geita.