KLABU HII INAFANYA MAMBO TOFAUTI IKIWA NI PAMOJA NA KUFANYA UBAINIFU WA CHANGAMOTO ZINAZOHUSU ELIMU NA KUTAFUTA MBINU ZA KUZITATUA AMA KUTOA USHAURI JUU YA UTATUAJI WA CHANGAMOTO.
KLABU HII INASIMAMIWA NA Ndg. AYUBU M. BWANAMADI AMBAYE NI MWALIMU KATIKA CHUO HICHO KWA UPANDE WA FANI YA UHAZILI (SECRETARIAL) AMBAYE PIA NI MWANAHARAKATI/RAFIKI WA ELIMU TANZANIA.
KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI (2014-2015) KLAMAEL ILIFANIKIWA KUPATA MAFANIKIO MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA KUPATA REDIO KUTOKA SHIRIKA LA HAKIELIMU LENYE MAKAO MAKUU YAKE MKOANI DAR ES SALAAM AMBAZO ZINATUMIA NISHATI YA JUA NA NGUVU MTU. REDIO HIZI ZINATUMIKA KAMA CHOMBO MUHIMU CHA KUPATIA TAARIFA MBALIMBALI ZA HABARI NA MATUKIO.
PIA BAADHI YA WANAKLABU AMBAO PIA NI WANACHUO KUPATA TONZO KUTOKA UONGOZI WA CHUO KWA KUPATA SIFA TOFAUTI IKIWA NI PAMOJA NA ELIMU.
KLABU HII ILIFANYA MKUTANO WAKE MKUU TAREHE 21 DESEMBA 2015 NA KUJADILI MAMBO TOFAUTI AMBAPO PIA WALIWEZA KUANDA TAARIFA MAALUMU KWA KIPINDI CHA MIAKA HIYO MIWILI




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni