Kurasa

Jumatano, 3 Juni 2015

MKUU WA MKOA ASISITIZA ELIMU

MKUU WA MKOA WA GEITA BI FATMA A. MWASA AMEWASISITIZA WAUMINI WA DINI YA UISLAMU KUSOMA NA KUSOMESHA WATOTO WAO ELIMU ZOTE ZINAZOWAKABILI IWE ILE YA DUNIA AU YA AKHERA (ELIMU YA DINI). MKUU HUYO ALIWASISITIZA WAUMINI WA DINI HIYO SIKU YA JUMAMOSI YA TAREHE 30 MAY 2015 KATIKA MAAULIDI YA KUADHIMISHA KUZALIWA KWA MTUMU MUHAMMADI SWALALLAH ALAYHI WASALAMU YALIYO FANYIKA KATIKA MSIKITI WA KATORO KIJIJI CHA KATORO WILAYANI GEITA MKOANI GEITA.

PIA MKUU WA MKOA WA GEITA ALIWASISI TIZA WATU WOTE WALIOHUDHURIA KATIKA MAADHIMISHO HAYO KUDUMISHA AMANI HASA KWA KIPINDI CHA UCHAGUZI TULICHOKUWANACHO NA KUHIMIZA KILA MWENYE SIFA YA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFRATI LA KUDUMU LA MPIGA KURA NI VEMA AKAJIANDIKA TENA KWA SIKU ZA MAPEMA ZAIDI.

PIA AKIWA NDIYE MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIZO ZA MAULIDI ALIZINDUA MRADI WA BOMBA LA MAJI AMBALO NI MSAADA MKUBWA KWA WAKAZI WA MAENEO YA KARIBU NA MSKITI MKUBWA WA KATORO NJE KIDOGO YA MJI WA GEITA.
PICHANI NI BI FATUMA A. MWASA AKIZINDUA MRADI WA BOMBA LA MAJI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni