HATIMAYE MARAFIKI WA ELIMU WA WILAYA YA GEITA WANAOUNDA MTANDAO WA MARAFIKI WA ELIMU WILAYA GEITA (
FENGD) WAMEFANIKIWA KUPITISHA KATIBA YAO HAPO JUMA MOSI YA TAREHE 06/06/2015 KATIKA KITUO CHA WALIMU KATORO
KATIBA YA MARAFIKI WA ELIMU (W) GEITA (FENGD),
TOLEO LA KWANZA 2015.
SEHEMU YA KWANZA:
1: UTANGULIZI:
IBARA YA 1: UTANGULIZI:
Sisi Marafiki wa
Elimu wilaya Geita {Friends Of Education Network Geita District} (FENGD) ambao ni muunganiko wa wanachama wa harakati za marafiki wa
elimu waishio katika wilaya ya Geita;
kwa hiari yetu tumeamua kujiunga kisheria ilil kushughulikia masuala ya
kuboresha Elimu, Demokrasia, Utawala
bora na mawasiliano katika jamii ya Geita kwa kushirikiana na wananchi wa kada
zote na wadau mbalimbali.
Asasi hii
imeanzishwa kwa matakwa ya wanaharakati wenyewe kwa lengo la kujihusisha na kuelimisha jamii ili kuboresha elimu na
demokrasia bila shinikizo toka kwa wana siasa, vikundi vya dini au ukabila.
Asasi hii itatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria za nchi kanuni na taratibu
za mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania.
IBARA YA 2: JINA LA KATIBA NA KUANZA KUTUMIKA:
2:1 Jina la Katiba.
Katiba hii ni waraka halali wa FENGD, hivyo itajulikana na kutambulika kwa jina la katiba ya “Marafiki wa Elimu (w) Geita (FENGD)”
2:2 Tarehe rasmi ambayo katiba hii itaanza kutumika.
Katiba hii itaanza kutumika mara baada
ya kupata usajli rasmi na wanachama wa FENGD
kufanya uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa katiba hii.
IBARA
YA 3: LUGHA YA ASASI:
Kwa kuwa FENGD ni asasi huru yenye wanachama wenye viwango tofauti vya
elimu; na kwakuwa FENGD inafanya
kazi na watu wa kada tofauti: lugha kuu ya mawasiliano itakuwa Kiswahili na
lugha ya pili itakuwa Kiingereza
SEHEMU YA PILI:
SEHEMU
YA II: KATIBA, USAJILI, ANUANI YA OFISI NA ENEO LA UTENDAJI KAZI:
IBARA
YA 4: Katiba
Katiba ya FENGD ndio muongozo wa shughuli zote za Asasi hii.
IBARA
YA 5: Jina la Asasi
Asasi hii itaitwa MTANDAO WA MARAFIKI WA ELIMU (W) GEITA kwa
kifupisho FENGD.
IBARA
YA 6: Usajili na Anuani
6:1 Baada ya kusajiliwa; makao makuu ya FENGD yatakuwa katka eneo lolote wilayani
Geita katika Jamhuriya Muungano wa Tanzania kulingana na makubaliano ya
wanachama.
6:2 Anuani ya FENGD itakuwa:-
Mtandao wa Marafiki wa Elimu Geita,
S.L.P
45, Geita.
IBARA
YA 7:
Eneo la utendaji kazi
FENGD itafanya kazi katika mkoa wa Geita
kwa kuhusisha ngazi mbalimbali za uanachama za FENGD.
IBARA
YA 8:
Washirika wa FENGD.
FENGD itakuwa na haki
ya kushirikiana na Taasisi, Mashirika mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, watu
binafsi, makampuni na Asasi nyingine ambazo zitakkuwa na nia ya kusaidia na kushirikiana na FENGD katika kutekeleza Dira na Dhamira
ya FENGD.
IBARA
YA 9: Kanuni za Kimaadili.
9:1 Katika
kutekeleza majukumu yake; FENGD itazingatia maadili, uadilifu, nidhamu, uwajibikaji
kujituma kujitolea na uchapakazi kwa manufaa ya taifa.
9:2 Wanachama na viongozi wa FENGD lazima
wawe waadilifu.
SEHEMU YA 3:
SEHEMU
YA III: DIRA, DHAMIRA, MADHUMUNI NA ULINZI WA ASASI:
IBARA
YA 10:
Dira ya FENGD:
Nikuwa na Geita yenye mazingira bora ya
elimu, utawala bora, Demokrasia ya kweli kwa wananchi wote mfumo bora na imara
wa mawasiliano ndani ya jamii.
IBARA
YA 11: Dhamira ya FENGD
Kuwezesha
upatikanaji wa taarifa sahihi kuhusiana na chamngamoto za elimu, Demokrasia na
Utawala bora na namna ya kushirikiana na serikali na jamii kuzikabili
changamoto hizo ilil kuleta mafabnikio chanya kwa manufaa ya umma.
IBARA
YA 12: Madhumuni ya FENGD.
12:1 Kufanya
ufatiliaji na uchambuzi wa masuala ya elimu, demokrasia, utawala bora na
kuimarisha mfumo wa mawasiliano katika jamii na vyombo vya utawala.
12:2 Kutoa
elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa ushiriki wao katika mikutano kwa manufaa ya
kijamii na kukabiliana na changamoto za maendeleo katika maeneo yao
12:3 Kuendesha
midahalo, mikutano, mijadala, na makongamano ya kijamii juu ya masuala mbalimbali
na kukabiliana na changamoto za maendeleo.
12:4 Kutumia vyombo vya habari kama redio, TV na
magazeti kuelimisha jamii
12:5 Kujihusisha
kikamilifu katika kusaidia jamii kitaaluma na ushauri katika masuala yanayo
kwamisha maendeleo yao
12:6 Kutoa
elimu kwa jamii hususani vijana wa shule za Msingi, Sekondari na vyuo pamoja na
walio nje ya shule kuhusiana na haki zao za msingi, elimu ya afya ya uzazi,
elimu kuhusiana na VVU/UKIMWI, magonjwa ya ngono, madhara ya matumizi ya dawa
za kulevya, elimu ya ujasiriamali na kuinua kipato, pamoja na masuala mtambuka kama mazingira n.k.
12:7 Kutoa
elimu ya Demokrasia na Utawala bora na Usawa wa kijinsia katika jamii.
12:8 Kuanzisha
club za Marafiki wa Elimu ndani na nje ya shule za msingi, sekondari na vyuo kwa
ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya elimu, demokrasia na utawala bora
katika jamii.
IBARA
YA 13: ULINZI WA ASASI:
Asasi
hii itatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na serikali ya
jamhuri ya muungano wa Tanzania; na dhamira
yake ya kutekeleza shughuli zake kwa mujibu wa katiba yake na sheria za
Tanzania.
SEHEMU YA 4:
SEHEMU
YA IV: AINA ZA UANACHAMA WA FENGD:
IBARA
YA 14: UANACHAMA.
Kutakuwa
na aina tatu tu za uanachama wa FENGD kwa mujibu wa katiba hii ambazo ni;
14: 1 Wanachama waanzilishi.
14.1.1 Huu ni uanachama wa watu walishiriki katika
kuanzisha wazo la kuundwa kwa
FENGD
na ambao kwa namna moja au nyingine walifanikisha FENGD kupata usajili.
14:2 Wanachama
binafsi
14.2.1 Huu ni uanachama wa mtu binafsi ambaye kwa
mapenzi yake atapendezwa na
shughuli
za FENGD na kuamua kujiunga kuwa mwanachama kwa hiari yake
mwenyewe.
14.2.2 Kwa mujibu wa katiba hii, kuwa mwanachama wa FENGD
katika wilaya
hakuunyimi
kuwa mwanachama mkoa wala Taifa.
14.3 Uanachama wa Heshima
14.3.1 Mtu binafsi, shirika, kampuni au Taasisi yoyote wanaweza kuwa
wanachama wa
FENGD
kwa kuchaguliwa /kuteuliwa na kamati kuu ya uongozi ya FENGD kisha
kuandikiwa barua
ya nia hiyo na iwapo watakubali watakuwa wanachama rasmi wa FENGD.
14.3.2 Mwanacham wa heshima wa FENGD hatapiga kura ya
maamuzi juu ya jambo lolote
linalohusu
FENGD.
IBARA
YA 15: SIFA ZA MWANACHAMA:
15:1 Wanachama
waanzilishi watatambuliwa kwa sifa zifuatazo:
15.1.1 Awe ni mtu aliyejitolea kwa hali na mali
katika kuanzishwa kwa FENGD
15.1.2 Awe na nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa
atakuwa mstari wa mbele kutimiza
Dira
na Dhamira ya FENGD.
15.1.3 Atambue kuwa anapaswa kuitumikia FENGD na si FENGD
imtumikie
15.1.4 Awe tayari kushirikiana na wadau wengine ili
kulinda maslahi ya taifa
15.2 Mwanachama
binafsi
15.2.1 Awe ni mtu mwenye kuziunga mkono kwa dhati shughuli na juhudi za FENGD
15.2.2 Awe mwenye kujitoa kuitetea FENGD ili kufanikisha
malengo yake
15.2.3 Awe na uwezo wa kuisaidia FENGD kwa hali na
mali pasipo kuchoka
15.2.4 Awe mtu yeyote mwenye akili timamu na umri
usiopungua miaka mitano (5)
IBARA
YA 16: HAKI ZA MWANACHAMA
Wanachama wa FENGD
wana haki zifuatazo.
16.1 Kuhudhuria vikao vinavyo wahusu kwa mujibu
wa katiba hii
16.2 Kupata taarifa ya FENGD kwa kufuata
taratibu zilizopo
16.3 Kushiriki
katika vikao mbalimbali vya maamuzi ya FENGD kwa mujibu wa taratibu
16.4 Kuchaguliwa au kuchagua viongozi wa FENGD
kwa mujibu wa wa taratibu za
Katiba.
16.5 Haki ya kujitetea na kujieleza kwa
tuhuma/kosa alilotenda mbele ya vyombo vya
FENGD.
16.6 Haki ya kuteuliwa kuiwakilisha FENGD katika
maeneo/ shughuli mbalimbali
16.7 Haki ya kupata taarifa na kuzitumia kwa
manufaa ya FENGD na jamii.
16.8 Haki ya kushiriki na kushirikisha uongozi
na wanachama wa FENGD katika mambo yenye manufaa kwa FENGD na jamii.
16.9 Haki ya kuwa na nakala ya katiba ya FENGD
IBARA
YA 17: WAJIBU WA MWANACHAMA:
Wajibu
wa mwanachama wa FENGDni pamoja na:,
17.1 Kulipa ada na michango yote ya FENGD kwa
ajili ya uendelevu wa Asasi
17.2 Kuhudhulia vikao na mikutano yote inayohusu
kwa mujibu wa katiba hii.
17.3 Kuwa mwaminifu, mwadilifu mkweli na kutetea
msimamo wa FENGD katika
Maendeleo.
17.4 Kuchangia mawazo kwa hali na mali katika
kulinda Dira na Dhamira ya FENGD.
17.5 Kufahamu kwa undani katiba ya mtandao
IBARA
YA 18: KUKOMA UANACHAMA:
Uanachama
utakoma kwa:
18.1 Mtandao wa wilaya kufutwa kwa mujibu wa
sheria za nchi
18.2 Mwanachama kuamua kujiudhulu kwa hiari yake
18.3 Kufukuzwa uanachama
18.4 Kushindwa kulipa ada kwa kipindi cha miaka
miwili mfululizo bila sababu za msingi
18.5 Kukiuka maadili ya uanachama wa FENGD kwa
makusudi
18.6 Kwa kutenda kosa lolote ambalo wanachama
wataridhia kwamba linafaa
kumuondoa
katika uanachama wa FENGD na uamuzi huo kuridhiwa na mkutano
mkuu.
SEHEMU YA TANO:
SEHEMU
YA V: MUUNDO NA WAJIBU WA VIONGOZI:
IBARA
YA 19: MUUNDO NA WAJIBU WA VIONGOZI:
Uongozi
wa FENGD utakuwa kama ifuatavyo
19.1 Mwenyekiti wa FENGD
19.2 Makamu mwenyekiti wa FENGD
19.3 Katibu wa
FENGD
19.4 Mratibu wa FENGD
19.5 Mweka hazina wa FENGD
19.1.0 Mwenyekiti
Wajibu wa
mwenyekiti utakuwa kama ifuatavyo:
19.1.1 Mwenyekiti ataongoza Mikutano ya Bodi ya
ushauri na mkutano mkuu wa
Wanachama
19.1.2 Mwenyekiti atakuwa msemaji mkuu wa FENGD
katika mikutano ya bodi ya ushauri
na
mkutano mkuu wa wanachama
19.1.3 Aache hisia zake binafsi zikiangalia maamuzi
ya wengi ila pale kunapokuwa na usawa wa maamuzi kwa pande mbili.
19.2.0 Makamu Mwenyekiti
19.2.1 Makamu mwenyekiti atafanya kazi za mwenyekiti kama mwenyekiti
hayupo
19.2.2 Atafanya kazi za mwenyekiti kwa kuagizwa
19.3.0 Katibu
Katibu
atakuwa na kazi zifuatazo;
19.3.1 Atatunza kumbukumbu za vikao vya bodi ya
ushauri na mikutano ya FENGD
19.3.2 Ndiye katibu wa mikutano ya kamati ya UBodi ya
Ushauri na mkutano mkuu wa
FENGD.
19.3.3 Katibu atawasiliana na mwenyekiti na makamu
mwenyekiti kwa maamuzi ya
utekelezaji
19.3.4 Kuandika barua na kuitisha vikao baada ya
kuwasiliana na mwenyekiti
19.3.5 Kuandaa agenda za mikutano ya Bodi ya Ushauri,
Mkutano mkuu na mikutano ya
Dharula
19.3.6 Kuandaa taarifa mbalimbali za FENGD na
kuzipeleka pale zinapohitajika
19.4 MRATIBU
19.4.1 Kuratibu shughuli mbalimbali za kamati ndogo
ndogo za FENGD
19.4.2 Kuratibu shughuli zote za kila siku za FENGD
19.4.3 Kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya mikutano
ya bodi ya ushauri na mkutano
mkuu
wa FENGD.
19.4.4 Kushughulikia suala la utafutaji wa
rasilimali fedha kwa ajili ya uendelevu
wa
FENGD
19.4.5 Ndiye mkuu wa kitengo cha mawasiliano na
utafiti
19.5.0 Mweka Hazina
Mweka
hazina atakuwa na wajibu ufuatao;
19.5.1 Atakuwa mtunzaji mkuu wa fedha za FENGD
19.5.2 Atasimamia utunzaji wa vitabu vya kumbukumbu
za fedha za FENGD
19.5.3 Ataandaa na kutoa taarifa za fedha za FENGD
katika vikao vya Bodi ya Ushauri na
Mkutano
mkuu wa FENGD.
19.4.4 Atakuwa mdhamini wa mali za Asasi kwa niaba ya
FENGD
SEHEMU YA SITA:
SEHEMU
YA VI: BODI YA USHAURI, MAMLKA NA MIKUTANO:
IBARA
YA 20: BODI YA USHAURI
20.0 Kuanzisha
Bodi
Kutakuwa
na bodi ya FENGD ambayo itajulikana kama “BODI
YA USHAURI”
Bodi
hii itaundwa na wajumbe tisa (9) na itadumu madarakani kwa muda wa
miaka
mitatu (3) na inaweza kuchaguliwa tena kuendelea na majukumu yake kwa
si zaidi ya vipindi
viwili.
20.1 Wajumbe wa Bodi.
Bodi
ya ushauri ya FENGD itakuwa na wajumbe kumi (10) ambao kati yao wanawake
watatu
(3) wajumbe watapatikana kama ifuatavyo:
20.1.1 Mwenyekiti wa FENGD
20.1.2 Makamu mwenyekiti wa FENGD
20.1.3 Mratibu ambaye pia ni Katibu wa FENGD
20.1.4 Mweka hazina wa FENGD
20.1.5 Wajumbe wawili (2) kutoka wanachama
waanzilishi wa FENGD
20.1.6 Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na mkutano
mkuu wa FENGD
IBARA
YA 21: WAJIBU, MAMLAKA NA KAZI ZA BODI
YA USHAURI
Bodi
ya Ushauri itakuwa na kazi na mamlaka kama ifuatavyo:
21.1.1 Itakuwa na mamlaka na madaraka ya kupokea
tarifa za utekelezaji wa kazi za
FENGD
21.1.2 Kutoa ushauri kwa uongozi na kutatua migogoro
ndani ya FENGD
21.1.3 Kufanya mapitio ya bajeti na kutoa maoni ya kuzingatiwa
na watendaji wa FENGD
21.1.4 Bodi ndio yenye mamlaka ya kuajiri watendakji
wa FENGD
IBARA
YA 22: MIKUTANO/VIKAO VYA FENGD NA MAJUKUMU YAKE.
FENGD
Itakuwa na Mikutano/vikao kama ifuatavyo;
22.1.0 Mkutano
Mkuu
22.1.1 Kutakuwa na mkutano mkuu wa wanachama ambao utafanyika mara moja
kila
mwisho
wa mwaka
22.1.2 Mkutano utahudhuliwa na watendaji wote wa FENGD,
wanachama hai (waliolipa
Kiingilio
na ada), wanachama waanzilishi wa FENGD, wanachama wa heshima na
wageni
mbalimbali watakao alikwa kuhudhulia
22.1.3 Mkutano mkuu ndio chombo chenye madaraka yote
ya kuamua mambo muhimu ya FENGD ikiwa ni pamoja na kupitisha sera na taratibu
mbalimbali za kusimamia uendeshaji wote wa Asasi
22.1.4 Kuchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti, mweka
hazina, na wajumbe wa bodi ya ushauri ya FENGD pamoja na wajumbe wa kamati
mbalimbali.
22.1.5 Kupokea na kupitisha makisio ya mapato na
matumizi ya FENGD kutoka kwa muweka hazina.
22.1.6 Kupitisha jina la mkaguzi wa mahesabu ya FENGD
22.1.7 Kujadili na kupitisha taarifa za mwaka za
utekelezaji wa shughuli za FENGD
22.1.8 Kujadili na kupitisha mabadiliko ya katiba ya FENGD
22.1.9 Kujadili na kupitisha mikakati yna mipango ya
muda mfupi na mrefu ya FENGD
22.1.10Kufanya
maamuzi yote ya FENGD, kama itakavyo onekana inafaa.
22.2.0 Mkutano
Mkuu wa dharura
22.2.1 Mkutano wa dharura unaweza kuitishwa endapo
kutakuwa na ombi lililotolewa na kutiwa saini na si chini ya theluthi mbili
idadi ya wanachama na kuweka bayana katika ombi hilo suala ambalo limesababisha
kuitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura.
22.2.2 Mkutano Mkuu wa dharura utahudhuliwa na
watendaji wote wa FENGD, wanachama hai (waliolipa ada na kiingilio), wanachama
waanzilishi, wanachama wa heshima na wageni waalikwa.
22.2.3 Mkutano Mkuu wa dharura unaweza kuitishwa mara
moja tu (1) kwa mwaka.
22.3.0 Bodi ya Ushauri
22.3.1 Bodi hii itakuwa na madaraka ya kuongoza na kusimamia kazi zote za FENGD
na
kazi
zote zitakazo elekezwa na mkutano mkuu.
22.3.2 Bodi hii itakuwa na madaraka ya kupitia
taarifa za utendaji/ utekelezaji za katibu
kwa
ajili ya kuziwasilisha kwenye mkutano mkuu
22.3.3 Kuratibu na kuongoza kazi za kamati ndogondogo
za FENGD na watendaji wake
22.3.4 Kuandaa rasimu ya marekebisho ya katiba kwa
ajili ya kujadiliwa na mkutano
Mkuu
22.3.6 Kuandaa rasimu ya sera na taratibu mbalimbali
kwa ajili ya kupelekwa kwenye
mkutano
mkuu kwa uthibitisho
22.3.7 Kuandaa rasimu ya mipango ya muda mfupi na
muda mrefu na bajeti ya kila
mwaka
kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za FENGD.
22.3.8 Kuandaa agenda na kuhakikisha kuwa mkutano
mkuu unafanyika kwa wakati
22.3.9 Kuandaa kamati ndogondogo za maeneo maalumu ya
utekelezaji.
22.3.10Kuitisha
mikutano ya Bodi na mkutano mkuu wa dharura si zaidi ya mara mbili tu
kwa
mwaka kama kuna ulazima wa kufanya hivyo
22.3.11Kuandaa
sheria ndogondogo na kanuni za FENGD.
SEHEMU YA SABA:
SEHEMU
YA VII: UENDESHAJI WA MIKUTANO NA VIKAO VYA FENGD
IBARA
YA 23: UENDESHAJI WA VIKAO:
23.1 Taarifa ya mkutano mkuu wa kawaida itatolewa
kwa kila mwanachama si chini ya siku kumi na nne (14), na taarifa ya mkutano mkuu wa dharura itatolewa kwa wanachama
si zaidi ya siku saba (7), kabla ya
siku ya mkutano husika.
23.2 Wanachama watakaotaka kuleta mawazo/ agenda
maalumu kwenye Mkutano Mkuu, watatoa taarifa ya maandishi kwa katibu wa FENGD
siku saba kabla ya siku ya mkutano.
23.3 Nusu ya idadi ya wanachama halali wa mkutano
mkuu watakamilisha akidi (Quorum) ya mkutano wowote ule isipokuwa kwamba akidi
haitahitajika endapo Mkutano umetokana na mkutano ulioahirishwa; endapo
wanachama watakao kuwepo watachukuliwa kutosheleza akidi.
23.4 Katika mkutano unaotokana na mkutano
ulioahirishwa hautaruhusiwa kufanya maamuzi yoyote ya kubadili katiba ya FENGD.
23.5 Endapo saa moja na nusu itapita tangu muda uliokubaliwa
kuwa ndio wa kuanza mkutano bila idadi ya wajumbe kutimia ili kuweza kufanya
mkutano; basi mkutano uta ahirishwa na Mwenyekiti au makamu mwenyekiti hadi
siku kama hiyo wiki inayofuata.
22.6
Mwenyekiti ndiye atakayeongoza mikutano ya Bodi, Kamati ya Utendaji, Mkutano
Muu na Mkutano Mkuu wa dharura.
22.7
Makamu mwenyekiti ataongoza shughuli za mikutano kama mwenyekiti hayupo.
22.8
EndapoMwenyekiti na makamu mwenyekiti hawakuhudhulia basi mjumbe mmoja anaweza
kupendekezwa kuwa mwenyekiti kwa wakati huo.
22.9 Katika mkutano mkuu maamuzi yatatokana na kupiga
kura kwa kuinua mikono juu isipokuwa kama wanachama walioko katika mkutano
wanamua kwamba kura zipigwe kwa siri (secret ballot).
22.10
Uamuzi utaonekena kuwa umepitishwa kwa idadi ya wingi wa kura kuunga mkono hata
kama tofauti ni ya kura moja (Majority decision) isipokuwa kama kura ni kwa
ajili ya kubadili katiba basi kura ni
lazima ziwe siyo chini ya theluthi mbili ya idadi ya wanachama waliohudhulia
kukubali.
22.11 Hakutakuwepo
na upigaji kura ya uwakilishi (no voting by proxy)
22.12
Katika upigaji kura endapo kura zitafungana Mwenyekiti atakuwa na kura ya Mwisho
(Casting vote)
22.13 Ni
budi Mwenyekiti aheshimiwe wakati wa mkutano
22.14 Uamuzi wa mwenyekiti katika kudhibiti
mwenendo wa mkutano ni wa mwisho labda kama atapingwa na theluthi ya wajumbe.
22.15 Mwenyekiti anamamlaka ya kuingilia usumbufu
wowote unaojitokeza wakati wa Mkutano au kumtoa nje mjumbe ambaye anasumbua
mwenendo wa mkutano.
22.16 Mjumbe
atakayetolewa nje kwa ajili ya usumbufu atatakiwa aondoke eneo la Mkutano.
SEHEMU YA NANE:
SEHEMU
YA VIII: UCHAGUZI NA MUDA WA KUKAA MADARAKAN.
24.0 Muda wa Uongozi
24.1 Viongozi watakao chaguliwa kwa mujibu wa
katiba hii watadumu madarakani kwa muda wa miaka mitatu (3), lakini wanaweza
kuchaguliwa tena.
IBARA
YA 25: SIFA ZA KIONGOZI:
25.1 Awe
mwanachama wa FENGD
25.2 Awe
na uwezo wa uongozi na kupambanua mambo
25.3 Awe
mwenye sifa na uwezo wa uongozi
25.4 Mwenye
kujituma
25.5 Anaye kubali kutoa na kupokea ushauri toka
kwa watu wengine walio wanachama na wasio wanachama wa FENGD na kuufanyia kazi.
25.6 Awe
tayari kujitolea kuliko kutegemea mapato/ malipo toka FENGD.
IBARA
YA 26: KUONDOKA KATIKA UONGOZI:
Viongozi
wanaweza kuondoka madarakani kwa njia zifuatazo;
26.1 Kutokuchaguliwa tena na wanachama
26.2 Kujiuzulu
26.3 Kupigiwa kura ya kutokuwa na imani
na wanachama
26.4 Kufukuzwa kutokana na makosa ya
kukiuka katiba hii
26.5 Kuhukumiwa kifungo jela kwa makosa
ya jinai n.k
26.6 Kupata maradhi ambayo yataathiri
kabisa uwezo wake wa kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
26.7 Kufariki dunia.
26.8 kuhama makazi ya kudumu nje ya
wilaya ya Geita
SEHEMU YA TISA:
SEHEMU
YA IX: MAPATO NA USIMAMIZI WAKE
IBARA
YA 27: MAPATO, UHIFADHI NA UTOAJI WA FEDHA BENKI:
27.1 Mapato ya FENGD yanatokana na ada za
uanachama, ada za kiingilio, michango ya wanachama, ruzuku na misaada ya
wafadhili/ wahisani mbalimbali wa FENGD.
27.2
Mwaka wa fedha wa FENGD utaanza tarehe 1 Januari na kuishia tarehe 31 Desemba ya
kila mwaka
27.3 Fedha zote za FENGD zitawekwa katika tawi la
benki litakalokuwa limeteuliwa isipokuwa fedha za matumizi madogomadogo
zisizozidi 50,000/= zitahifadhiwa kwenye ofisi ya FENGD (Kama Petty Cash).
27.4 Waweka saini benki watakuwa wane (4) ambao ni
Mwenyekiti, Muhasibu na wajumbe wawili watakao chaguliwa na Bodi yaUshauri
ambapo kati yao wawili watakuwa kundi “A”na wawili watakuwa kundi “B”.
27.5 Fedha zitatolewa benki kwa kusainiwa na watu
wawili mmoja kutoka kundi A na mmoja kutoka kundi B.
SEHEMU YA KUMI:
SEHEMU
YA X: MABADILIKO YA KATIBA, KUVUNJIKA NA LAKIRI YA ASASI.
IBARA
YA 28: MABADILIKO YA KATIBA, KUVUNJA NA LAKIRI YA ASASI:
28.0 Mabadiliko ya Katiba:
28.0.1 Katiba haiwezi kubadilishwa au kufanyiwa
marekebisho kwa namna yoyote ile isipokuwa kwa uamuzi utakaokuwa umefikiwa
katika Mkutano Mkuu maalumu wa wanachama ambao utahudhuliwa na si chini ya
theluthi mbili ya wanachama.
28.1 Kuvunjika
kwa Asasi
28.1.1 FENGD itafikia ukomo kwa kuvunjika kama uamuzi
huo utafikiwa na theluthi mbili ya wanachama waliohudhulia Mkutano Mkuu kupiga
kura za kukubali uamuzi huo
28.1.2 Kama Mkutano utaazimia kuvunjika kwa FENGD;
Bodi ya Ushauri itafanya utaratibu wa kulipa madeni yote ya FENGD na hatimaye
kumilikisha mali za FENGD kwa asasi yenye makao yake mjini Geita na yenye
malengo yanayofanana na ya Asasi hii.
IBARA
YA 29: MUHURI NA NEMBO YA FENGD:
29.1 Kutakuwa na muhuri wa Asasi ambao ni wa
duara na ndani yake utasomeka MARAFIKI WA ELIMU (W) GEITA na katikati ya maneno
hayo kutakuwa na anuani ya FENGD, S.L.P. 45 GEITA.
29.2 Nembo ya FENGD.
29.2.1 Nembo ya utambulisho ya FENGD itakuwa na watu
wazima wawili wa jinsia zote walioshikana mikono kuwafunika watoto wawili wa
jinsia zote na nyuma ya watoto kutakuwa na kitabu chenye kalamu katikati.
29.2.2 Maana ya kuwa na alama hizi ni kwamba kwa kuwa
na elimu; kutakufanya kuona mbali, kuwa na upeo mzuri wa matumizi ya anga,
kutumia vyema rasilimali za nchi kavu na baharini kwa manufaa ya Taifa.
29.2.3 Kwenye nembo hiyo kutakuwa na maneno
yanayosomeka Mtandao Wa Marafiki Wa Elimu
(w) Geita * Friends Of Education Network Geita District (FENGD).
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
SEHEMU
YA XI: MENGINEYO:
IBARA
YA 30: UWEZO WA KUJIUNGA NA TAASISI NYINGINE:
30.1 FENGD inaweza kujiunga
na Asasi na Taasisi nyingine kwa kadri inavyofaa ili mradi uamuzi wa kujiunga
na Taasisi au mitandao utaafikiwa na Bodi na wanachama watapata taarifa hizo
kupitia kwenye Mkutano Mkuu.
IBARA
YA 31 UTATUZI WA MIGOGORO:
31.1 Mgogoro wowote ndani ya FENGD utakaoshindikana
kupata usuluhishi ndani ya FENGD, utaamuliwa na wanachama wa FENGD katika
Mkutano Mkuu na huo ndio utakuwa na madaraka na maamuzi ya mwisho.
UTHIBITISHO:
Sisi ambao majina yetu yameorodheshwa
hapa chini na kutiwa saini zetu ndio wanachama waanzilishi wa Asasi ya Marafiki
wa Elimu (w) Geita (FENGD) mwaka 2015. Kwa kutambua kuwa jamii inategemea
juhudi za watu mbalimbali wenye ushirikiano ili kuleta maendeleo; tumeamua kwa
ridhaa yetu kufanya uamuzi wa kuanzisha Asasi hii ambayo itafanya kazi kwa
ushirikiano na jamii, wataalam mbalimbali na wadau kutoka serikalini na wadau
wanje ili kufikia malengo ya FENGD na maendeleo ya Taifa.
Tutailinda, kuiheshimu na kuitunza
Katiba hii ili itekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu
za kisheria za Tanzania.
No
|
JINA
|
SAINI
|
1
|
|
|
2
|
|
|
3
|
|
|
4
|
|
|
5
|
|
|
6
|
|
|
7
|
|
|
8
|
|
|
9
|
|
|
10
|
|
|
11
|
|
|
12
|
|
|
13
|
|
|
14
|
|
|
15
|
|
|
TUNATHIBITISHA
KWAMBA HII NI NAKALA HALISI YA KATIBA YA FENGD
**********************************************************************
MUUNDO WA FENGD